Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-SIASA

Burundi yaomba UN kubadili wafanyakazi wake

Katika taarifa iliyorushwa hewani kwenye redio ya taifa, Makamu wa Kwanza Rais Gaston Sindimwo amesema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi wanapotoshwa na wanasiasa na hivyo kutoa ripoti sizizokuwa na msingi.

Viongozi wa Burundi waomba kubadilishwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura.
Viongozi wa Burundi waomba kubadilishwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Gaston Sindimwo pia amesema kuwa "matatizo ya Burundi husababishwa na wageni ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa". "Hii ndiyo sababu inayopelekea sisi kumuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kubadili wafanyakazi wa taasisi hiyo ya kimataifa waliopo hapa Burundi, na hivyo kukosoa ripoti walizozitoa hapo awali," Gaston Sindimwo amesema.

Kauli hii ya Gaston Sindimwo inakuja siku moja baada ya ombi la vikwazo dhidi ya wale waliohusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Burundi.

Katika barua iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Mashirika 19 ikiwa ni pamoja na Human Rights Watch, Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) na mashirika yanaoendesha harakati zao nchini Burundi ACAT Burundi na shirika linaloteta Haki za Binadamu na za wafungwa (APRODH) yamebaini kwamba kuwa vikwazo hivi huenda vikatoa ujumbe mzito kwa viongozi wa Burundi.

Tangu mkuanza kwaa mgogoro uliosababishwa na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, machafuko yaliyofuata yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.

Mapema wiki hii, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Mauaji ya Kimbari Adama Dieng alionya dhidi ya hatari ya vurugu kubwa kutokea nchini Burundi.

Hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alielezea wasiwasi wake katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki chache zilizopita.

Lakini serikali ya Burundi imetaja taarifa hizi kuwa ni uzushi mtupu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.