Pata taarifa kuu
RFI-BURUNDI-WAKIMBIZI

Wanahabari wa RFI watoa msaada kwa wakimbizi wa Burundi

Waandishi wa Habari wa Radio France International wametoa zawadi kwa watoto kutoka Burundi ambao wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Lusenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakimbizi 400 kutoka Burundi wakipokelewa katika kambi ya muda mjini Uvira, DRC, Mei 4, 2015.
Wakimbizi 400 kutoka Burundi wakipokelewa katika kambi ya muda mjini Uvira, DRC, Mei 4, 2015. RFI/LL.WESTERHOFF
Matangazo ya kibiashara

Zawadi hizo zitakabidhiwa kwa watoto hao kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wakimbizi UNHCR.

Kambi hiyo iliyo Kilomita 70 kutoka mpaka wa Burundi, inawapa hifadhi wakimbizi zaidi ya elfu 20 tangu mwaka 2015.

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi umesababisha maelfu ya raia kuyahama makaazi yao na kukimbilia nchi jirani, hususan nchini Tanzania, Rwanda, DR Congo, Kenya, Uganda, Zambia, na wengine wenye uwezo katika nchi za Ulaya na Marekani.

Watu zaidi ya 1000 wameuawa tangu mgogoro huo kuzuka kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.