Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Polisi 2,500 watumwa katika kaunti ya Baringo

Serikali ya Kenya imetuma zaidi ya polisi katika Kaunti ya Baringo, kaunti ambayo wafugaji kutoka jamii za Pokot na Turkana wamekuwa wakishambuliana.

Serikali ya Kenya yatuma polisi 2500 kuzima ghasia katika kaunti ya Baringo.
Serikali ya Kenya yatuma polisi 2500 kuzima ghasia katika kaunti ya Baringo. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo pamoja na wizi wa mifugo, yamesababisha zaidi ya watu elfu nne kusalia wakimbizi na watu wengine 10 kupoteza maisha wakiwemo wanasiasa wawili waliopigwa risasi.

Naibu rais William Ruto amesema serikali itatoa Dola za Marekani 970,000 kuwafidia wale wote waliopoteza mifugo yao.

Mashahidi wanasema kuwa uchaguzi ambao utafanyika mwezi Agosti umechangia kuchochea hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.