Rais wa ICC atembelea watu walioteswa na LRA nchini Uganda
Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC Jaji Silvia Fernandez de Gurmendi anazuru Kaskazini mwa Uganda, kukutana na waathiriwa walioteswa mikononi mwa waasi la Lords Resistance Army.
Imechapishwa:
Waathiriwa hao wanasaidiwa kujikwamua kiuchumi na Shirika moja la Kimataifa linaloshirikiana na Mahakama ya ICC.
Ziara hii inakuja wakati huu Kamanda wa juu wa kundi la LRA Dominic Ongwen kesi yake ikiendelea katika Mahakama hiyo mjini Hague nchini Uholanzi.
Inaarifiwa kuwa kundi la LRA lilihusika na mabaya mengi nchini Uganda na katika nchi jirani, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, uporaji, mateso kwa raia na watoto kutumiwa katika kundi hilo kama wapiganaji.