Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Mkuu wa UN amuonya rais wa Burundi kuhusu muhula wa nne

Katibu Mkuu wa Umoja Antonio Guterres amemuonya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza dhidi ya kutafuta muhula wa nne madarakani akisema hatua hiyo inahatarisha kuongezeka kwa mgogoro katika nchi za Afrika.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyopatikana na AFP, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anasema ana wasiwasi sana na kauli za hivi karibuni za rais Nkurunziza, ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2005, na zinazopendekeza aweze kutafuta muhula wa nne kuwa madarakani hatua ambayo itahitaji mabadiliko ya katiba.

Katika ripoti aliyoituma kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi Guterres amesema kuwa jaribio la rais Nkurunziza kutafuta muhula wa nne chini ya hali ya sasa kutahatarisha kuongeza mzozo na kudhoofisha juhudi za pamoja kutafuta suluhu ya kudumu.

Malefu ya watu wamepoteza maisha katika vurugu nchini Burundi zilizochochewa na uamuzi wa rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwaka 2015 uchaguzi ambao alishinda.

Watu wapatao 387 wamekimbia nchi hiyo na idadi inatarajiwa kuongezeka na kuzidi 500,000 mwaka huu 2017 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la wakimbizi UNHCR.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.