Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yawataka wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo kuwasilisha vibali vyao

Serikali ya Tanzania imetoa muda wa mwezi mmoja kwa raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo, kufika katika Wizara ya Kazi na kuwasilisha vibali vyao vya kufanya kazi na kuishi ili vikaguliwe.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Kazi nchini humo imesema imechukua hatua hii baada ya kubaini kuwa, wageni wengi wanaoishi na kufanya kazi nchini humo wamekuwa wakipata vibali bila ya kufuata utaratibu mwafaka.

Baada ya muda huo kumalizika, Wizara hiyo imetangaza kuwa itafanya msako wa kitaifa kuhakikisha kuwa raia wote wa kigeni wanakuwa na vibali sahihi.

Wiki mbili zilizopita, idara ya uhamiaji nchini humo ilimtuhumu Mfanyibiashara maarufu Yusuf Manji, kuwaajiri wafanyakazi wa kigeni wasiokuwa na kibali.

Ukiwaondoa raia wengine wa kigeni, mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unazitaka nchi zote sita kuwaruhusu raia wake kutembea na kufanya kazi bila ya usumbufu wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.