Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Nusu ya raia wa Sudan Kusini wanakabiliwa na baa la njaa

Serikali ya Sudan Kusini inasema nusu ya raia wake wapatao Milioni tano wanakabiliwa na baa la njaa.

Msichana mdogo akionekana akiwa amebeba beseni za maji, inakadiriwa wasichana milioni 10 barani Afrika wanafanya kazi zisizo na malipo.
Msichana mdogo akionekana akiwa amebeba beseni za maji, inakadiriwa wasichana milioni 10 barani Afrika wanafanya kazi zisizo na malipo. UN Photo/Eskinder Debebe
Matangazo ya kibiashara

Isaiah Chol Aruai, Mwenyekiti wa Shirika la taifa linaloshughulikia takwimu, amesema hali hiyo imechangiwa sana na machafuko yanayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Jimbo lililoathiriwa zaidi na baa hili ni lile la Unity, ambalo raia katika eneo hilo wanaendelea kuteseka kwa kukosa chakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu kama maji na huduma za afya.

Vita kati ya wanajeshi wa serikali na makundi ya waasi, vimesababisha bei ya vyakula kupanda maradufu na kiwango duni cha uzalishaji wa mazao kwa sababu watu wameyakimbia makwao na kuacha mashamba yao kwa kuhofia vita.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na maswala ya kibinadamu nchini humo Eugene Owusu, amesema janga hili limesababishwa na hali mbaya ya kisiasa na uongozi nchini humo.

Mapigano nchini Sudan Kusini yamesababisha maelfu ya raia kukimbilia katika nchi jirani kama Uganda na Kenya.

Viongozi wa kisiasa nchini humo rais Slava Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wameshindwa kutekeleza mkataba wa amani waliokubaliana mwaka 2015 jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.