Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA

Benjamin Mkapa kukutana na wanasiasa wa Burundi

Mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa anatarajiwa kukutana na wanasiasa wa nchi hiyo wakati huu mazungumzo hayo yaliyosusiwa na serikali yakiingia siku yake ya pili.

Kikao cha pili cha mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi kinafanyika mjini Arusha, Tanzania.
Kikao cha pili cha mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi kinafanyika mjini Arusha, Tanzania. Photo: Wikimedia/Phase9
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa Burundi wanakutana tangu Alhamisi wiki hii mjini Arusha nchini Tanzania chini ya mratibu wa mazungumzo hayo ya amani, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Mgogoro huo umesababisha maelfu ya raia wa Burundi kulitoroka taifa lao na wengine wanaokadiriwa kufikia elfu moja kupoteza maisha kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

Wakati mazungumzo ya amani ya Burundi yakianza jijini Arusha nchini Tanzania makundi mbalimbali ya kijamii toka nchini Burundi yametaka kuwepo kwa ushirikishwaji mpana hasa kwa wanawake na makabila mengine madogo nchini humo, ikiwa ni pamoja na kundi la watu kutoka jamii ya Waswahili. Polisi ya Tanzania ilijitahidi kuzima maandamano ya watu hao na kuwakamata baadhi yao Alhamisi wiki hii.

Serikali ya Burundi ilisema haitashiriki katika mazungumzo ya amani yaliyoanza Alhamisi wiki hii kati yake na wanasiasa wa upinzani, mjini Arusha nchini Tanzania.
Hata hivyo muungano wa wanasiasa wa upinzani CNARED unashiriki katika mazungumzo hayo.

Awali Msemaji wa serikali Philippe Nzobonariba alisema Bujumbura haijaridhiswa na namna mazungumzo haya yalivyoandaliwa lakini pia uwepo wa mshauri wa Umoja wa Mataifa Benomar Jamal.

Hatua hii ya serikali ya Burundi, inarudisha nyuma upatikanaji wa suluhu kuhusu mzozo wa kisiasa nchini humo hasa wakati huu ambao muungano wa vyama vya upinzani CNARED ambao viongozi wake wanaoishi nchi wakikubali kuhudhuria mazungumzo hayo, yanayoongozwa na Mratibu ambaye ni rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.

Rais mstaafu wa Tanzania anataka kujadiliwa kwa mara ya kwanza "masuala nyeti", kama vile muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza unaoendelea kuzua utata na "uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa," amesema mwanadiplomasia wa Afrika ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Majaribio ya kuwaleta kwenye meza moja ya mazungumzo serikali ya Burundi na upinzani walio uhamishoni hadi sasa yameshindwa. Serikali ya Bujumbura imekataa mpaka sasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na Cnared licha ya shinikizo na vikwazo kutoka jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.