Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani nchini Kenya waonya kutokubaliana na wizi wa kura

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameonya kuwa, wizi wa kura hautakubaliwa nchini humo baada ya wakenya kupiga kura mwezi Agosti.

Kinara wa upinzani Raila Odinga (Kushoto) akiwa na katibu mkuu wa chama cha KANU.
Kinara wa upinzani Raila Odinga (Kushoto) akiwa na katibu mkuu wa chama cha KANU. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi imeahidi kuwa itasimamia zoezi hilo kwa haki ili mshindi wa Uchaguzi wa urais atakayetanagzwa mshindi anakubaliwa na wote.

Wakati huo huo Jaji wa Mahakama Kuu Chache Mwita ameigiza Tume ya Uchaguzi kuendelea na zoezi la kuwaandikisha wapiga kura wapya hadi siku ya Jumapili.

JE, hatima ya Kenya katika uchaguzi wa 2017 ni ipi? Hili ni swali sugu ambalo kila Mkenya anasubiri jibu lake kwa hamu. Uchaguzi wa urais ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi yoyote. Ni ndoto ya kila mmoja kuishi katika maeneo yenye haki, usawa na amani. Kenya inapitia hatua muhimu inapojiandaa katika uchaguzi wa urais wa 2017.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)

Hii ni tume ambayo hujihusisha na shughuli za kuhesabu kura katika uchaguzi nchini Kenya. Mnamo Mei 2016, kulikuwa na ghasia zilizotokana na maandamano katika mji mkuu wa Nairobi na kusababisha vifo vya watu watatu.

Maandamano haya yalisababishwa na wafuasi wa chama cha CORD ambacho kinara wake ni Raila Odinga. Sababu kuu ya maandamano hayo, ni kwamba walitaka serikali ifanye mabadiliko katika tume hii ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

IEBC ilidaiwa kuunga mkono chama tawala na kupanga kukisaidia kwa kutumia ulaghai kwenye uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika mwaka ujao. Kufuatia hayo, IEBC ilitakiwa kujiuzulu na viongozi wa upinzani wa CORD. Upinzani ulihisi kwamba, makamishna wa IEBC walihusika na udanganyifu wa kura za urais mwaka 2013.

Hatimaye, makamishna wa Tume huru ya Uchaguzi Kenya, walisema wako tayari kujiuzulu. Makamishna hao tisa, wakiongozwa na mwenyekiti wao, Isaac Hassan, waliafiki uamuzi huo mbele ya kamati ya pamoja katika Bunge la Taifa na Seneti, iliyobuniwa kupokea shutuma dhidi yao na pia mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha shughuli za uchaguzi nchini Kenya.

Maandalizi ya Jubilee

 Rais Uhuru ana mpango upi ili apate ushindi katika uchaguzi wa urais wa 2017? Chama cha Jubilee ni mojawapo ya vyama vinavyovuma nchini Kenya kisiasa. Kinara wa Jubilee ni Rais Kenyatta.

Mojawapo ya mipango yao katika uchaguzi wa Urais wa 2017, ni kufungua ofisi  zao katika kaunti 47. Rais Kenyatta ana kibarua kikubwa katika kukipigia debe chama chake katika kaunti hizi.

Kuna mpango tayari wa kuhakikisha kwamba vyama vidogo vinavyounda Jubilee vinakubaliana kuhusu maofisa wa chama hicho kote nchini.

Mnamo Septemba 10, mwaka huu, Rais  Kenyatta pamoja na Naibu wake, William Rutto, walizuru uwanja wa Kasarani mjini Nairobi na kukutana na wafuasi wao.

Katika eneo la Magharibi mwa Kenya, litakuwa jukumu la vyama kama vile New Ford Kenya (NFK) na United Democratic Front (UDF), kuafikiana kuhusu watakaoteuliwa kuwa maofisa wa chama cha Jubilee.

Kando na hayo, wenyeviti kutoka matawi 47, watatengeneza baraza kuu la Jubilee Party, ambalo litaendesha shughuli za kila siku za chama. Wanasiasa wawili kutoka maeneo yote nane watafanya kazi pamoja na Rais Kenyatta na Naibu wake Rutto, ili kutengeneza kamati kuu tekelezi ya chama.

Kulingana na ripoti iliyochapishwa katika mtandao wa habari wa Star, Rais Kenyatta na Naibu wake watazuru kaunti 47 ili kukutana na viongozi wa vyama na kukiuza chama hicho kabla ya uchaguzi wa 2017. Ziara hizo za kaunti zitaanza mwishoni mwa mwaka huu.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee Kenya State House

Raila Odinga amejiandaa vipi?

Kinara wa chama cha ODM, Odinga, kwa muda mrefu amekuwa akitoa upinzani kwa chama tawala. Ilikuwa bahati mbaya sana kwake, kwani kila mara amekuwa akishindwa kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu.

Inapendeza sana jinsi bingwa huyu wa siasa hafi moyo kisiasa, kwani anaonekana kila mara akiinyooshea serikali mkono wa lawama iwapo kumetokea sakata lolote la wizi au utenda kazi hafifu.

Katika chama hiki cha ODM, kulikuwa na mvutano kuhusu nani anastahili kupeperusha bendera ya muungano huo, dhidi ya muungano wa Jubilee.

Hata hivyo, katika mahojiano nyumbani kwake kule Karen Nairobi, Raila alisema kwamba yuko tayari kumuunga mkono yeyote atakayesimamia kiti cha ugombea urais katika chama cha ODM ili kumshinda Kenyatta.

Kiujumla Rais Kenyatta amejaribu kila awezavyo kuwa kiongozi bora. Hata hivyo, serikali yake imekumbwa na changamoto nyingi sana, mojawapo ikiwa ni ufisadi, ugaidi na mengine mengi. Wakenya wengi wanamtizama kwa jicho la karibu sana kulingana na namna anavyojaribu kukabiliana na changamoto hizo.

Viongozi wa fedha wa mataifa mbalimbali ulimwenguni wamempongeza Rais Kenyatta kwa mtazamo na uongozi bora ambao wanasema ni muhimu katika ukuaji wa bara la Afrika.

Kiongozi wa Benki ya Dunia na African Development Bank (AFDB) alisema sera za Kenya zilizoanzishwa na Rais Kenyatta zimeweka mazingira mazuri ambayo yamechangia uwekezaji na biashara kati ya mataifa ya Afrika.

Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama
Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama mbunge anayehojiwa na vyombo vya usalama REUTERS/Goran Tomasevic

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.