Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA

Mvutano wajitokeza kabla ya mazungumzo ya amani nchini Burundi

Wakati ikisalia siku moja tu kabla ya kuitishwa duru nyingine ya mazungumzo baina ya wadau wa siasa ya Burundi mjini Arusha nchini Tanzania, tayari swala la watakaoshiriki mazungumzo hayo limeanza kuzua sintofahamu.

Askari polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Februari 3, 2016.
Askari polisi wakipiga doria katika mtaa wa mji wa Bujumbura, Februari 3, 2016. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo muungano wa vyama vikuu vya upinzani (CNARED) pamoja na kuwa haukualikwa kama kundi, unasema umetuma wawakilishi wake kuhudhuria mkutano wa siku ya Alhamisi.

Katika hatua nyingine, waziri wa mambo ya ndani wa Burundi, Pascal Barandagiye, amesafiri hadi nchini Uganda kwenda kuwashawishi raia wake warudi nyumbani kwa kuwa amani imerejea.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa mvutano huu huenda ukapunguza kasi ya kupatikana kwa suluhu baina ya pande hasimu kama mratibu wa mazungumzo alivyopendekeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.