Pata taarifa kuu
TANZANIA-MIHADHARATI

Rais Magufuli atangaza vita dhidi ya mihadarati

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ameitaka polisi na jeshi kuongeza juhudi katika vita dhidi ya dawa za kulevya ili kuhakikisha sheria imesimamiwa ipasavyo kwa kukabiliana na tatizo hilo sugu nchini Tanzania.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli akiagiza vyombo vya usalama na ulinzi katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli akiagiza vyombo vya usalama na ulinzi katika vita dhidi ya madawa ya kulevya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Rais Magufuli amewataka viongozi wote wa serikali kuungana na vyombo vya usalama na ulinzi katika vita dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya mihadarati.

“Sitaki mapambano hayo yafanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza. Kuna ulazima hapa wa kila mmoja kuheshimu sheria na kazi anayoifanya ” amesema Rais wa Tanzania.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo hii leo katika Ikulu ya mjini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kumuapisha Kamishna mkuu wa taasisi ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Rogers Siyanga.

Wakati huo huo Kamishna Jenerali wa uhamiaji Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Grace Aaron Mgovano wmeapishwa pia.

Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza operesheni ya kukamata watu wanaojihusisha na biashara za mihadarati, na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudu za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya.

Hivi karibuni kikosi cha polisi nchini Tanzania kiliwasimamisha kazi kwa muda maafisa 12 wa polisi ambao ni miongoni mwa wale waliotajwa na kamishna wa polisi wa jimbo la Dar es Salaam bw Paul Makonda miongoni mwa watu wanaoshirikishwa na ulanguzi wa mihadatari.

Kamishna wa polisi Paul Makonda alisema kuwa uchunguzi unaendelea dhidi ya idadi kubwa ya wasanii ambao pia aliwataja na kuripoti katika vituo vya polisi ili kuhojiwa.

Kulingana na Gazeti la The Citizen nchini humo Inspekkta Jenerali Ernest Mangu alisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya maafisa hao 12 uchunguzi utakapokamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.