Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Rais Uhuru Kenyatta atia saini mabadiliko tata ya sheria ya Uchaguzi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini mswada tata wa mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta akitia saini mswada wa sheria katika Ikulu ya Nairobi
Rais Uhuru Kenyatta akitia saini mswada wa sheria katika Ikulu ya Nairobi State House Nairobi
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inamaanisha kuwa Tume ya Uchaguzi nchini humo IEBC sasa itaamua ni mfumo upi mbadala wa kutumia kuwatambua wapiga kura na kujumuisha matokeo ikiwa mfumo wa Kieletroniki utagoma.

Sheria hii inapingwa vikali na wanasiasa wa upinzani wanaodai kuwa mabadiliko hayo yanatoa mwanya kwa serikali kuiba kura, madai ambayo serikali inakanusha na kusisitiza kuwa mabadiliko hayo yalipendekezwa na Tume ya Uchaguzi.

Bunge la Senate wiki iliyopita, lilipitisha mabadiliko hayo baada ya bunge la kitaifa kufanya hivyo mwezi Desemba mwaka uliopita, licha ya wabunge wa upinzani kuondoka bungeni baada ya kuzuka kwa mvutano mkali.

Upinzani unasisitiza kuwa kama njia mbadala itatumika, basi iwe ni ya eletroniki, ili kuzuia wizi wa kura.

Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, wanatarajiwa kuwa na kikao cha pamoja siku ya Jumatano jijini Nairobi, kuchukua msimamo wa pamoja baada ya mabadiliko hayo kupitishwa na Bunge la Senate.

Sheria hii mpya, imeonekana kuligawa taifa hilo kisiasa wakati huu kukiwa na wito wa kufanyika kwa mazungumzo zaidi ili kupata mwafaka.

Upinzani umekuwa ukisema kuwa hautashiriki katika Uchaguzi huo ikiwa sheria hii haitabadilishwa.

Wakati uo huo Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa, itaanza zoezi la kuwasajili wapiga kura zaidi ya Milioni 6, kuanzia wiki ijayo kabla ya Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.