Pata taarifa kuu
TANZANIA

Wanasheria wanawake nchini Tanzania watakiwa kupambana na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaagiza majaji na mahakimu wanawake kote nchini Tanzania kupambana ipasavyo katika kukabiliana na vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii. 

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suhulu Hassan
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suhulu Hassan 3.bp.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Makamu huyo wa Rais ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nane wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA).

Aidha ameonya kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo ni mbaya na lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.

Amesema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.

Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha Majaji Wanawake (IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika programu ya miaka mitatu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.