Pata taarifa kuu
KENYA-UTALII

Maelfu ya watalii wazuru Kenya baada ya usalama kuimarishwa

Maelfu ya watalii wanazuru Pwani ya Kenya kipindi hiki cha Sikukuu, huku wamiliki wa Hoteli na Migahawa wakisema biashara ni nzuri, hoteli zimejaa kinyume na ilivyokuwa mwaka uliopita. Usalama nao umeimarishwa pwani ya nchi hiyo.

Utalii unaiingizia Kenya zaidi ya Euro milioni 540 kwa mwaka.
Utalii unaiingizia Kenya zaidi ya Euro milioni 540 kwa mwaka. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Wadau wa utalii ukanda wa pwani ya Kenya wanasema idadi ya watalii wanaozuru eneo hilo imeongezeka kwa kiasi kikubwa msimu huu, kutokana na juhudi za wadau wa utalii kuuza sifa za sekta hiyo ndani ya nchi hiyo na hata katika soko la kimataifa.

Kulingana na wadau wa sekta hiyo ukanda wa pwani, asilimia 90 ya hoteli za watalii zimejaa watalii kufikia sasa huku idadi ya watalii wa ndani ikiongezeka hadi asilimia 50, huku asilimia 50 ikiwa ni ya watalii wa kimataiafa waliozuru ukanda huo.

Baadhi ya watalii kutoka eneo la Kiambuu mkoa wa kati hapa nchini, waliozuru mjini Mombasa wanasema wamefurahishwa na maandhari safi na mazingira tulivu ya pwani, pamoja na hali ya usalama ilivyo.

Serikali inasema juhudi za vyombo vya usalama kuweka usalama thabiti nchini zimechangia pakubwa utalii kuimarika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.