Pata taarifa kuu
UGANDA

Kikosi cha kupambana na ugaidi chafanya msako Msikiti wa Nakasero jijini Kampala

Kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini Uganda, kimevamia msikiti wa Tabliq Nakasero jijini Kampala Jumanne asubuhi.

Msikiti wa Tabliq Nakasero jijini Kampala
Msikiti wa Tabliq Nakasero jijini Kampala wordpress.com
Matangazo ya kibiashara

Habib Buwembo mmoja wa wasemaji wa Msikiti huo amesema maafisa hao walivunja milango ya Ofisi ya msikiti huo na kuchukua Kompyuta pamoja na stakabadhi muhimu.

Aidha, amesema walinzi 11 walikamatwa wakati wa msako huo na hawajulikani waliko.

Msemaji wa Polisi Andrew Felix Kaweesi amethibitisha kufanyika kwa msako huo na kueleza kuwa maelezo ya kina yatatolewa katika siku zijazo.

Haijafahamika ikiwa msako huu, unahusishwa na kukamatwa kwa viongozi wakuu wa dhehebu la Kiislamu la Jamat Dawatil Salafiya.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi katika Msikiti huo baada ya kukamatwa kwa viongozi wa dhehebu hilo akiwemo, Sheikh Yahaya Mwanje na Katibu Mkuu Ayub Nyende miongoni mwa wengine.

Uganda imekuwa ikikabiliwa na mauaji ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu akiwemo Hassan Kirya, msemaji wa dhehebu la Kibuli, Amir wa zamani wa jiji la Kampala Mustafa Bahiga na Mhubiri wa Kishia Abdul Qadir Muwaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.