Pata taarifa kuu
KENYA-ICC

Kenya kutathmini jinsi ya kuondoka katika ICC

Serikali ya Kenya itathmini wazo la kuondoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), amesema Jumatatu hii Desemba 12 Rais Uhuru Kenyatta, alipokua akiwahutubia wananchi katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa nchi yake. Kenya itakua nchi ya nne, baada ya Burundi, Gambia na Afrika Kusini.

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto, Aprili 4, 2015 mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto, Aprili 4, 2015 mjini Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa haijajulikana iwapo serikali ya Kenya na Bunge pamoja na baraza la Seneti watapitisha wazo hilo la kuondoka katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

"Uzoefu wetu na ICC unaonyesha kuwepo kwa ukosefu wa uadilifu ndani ya taasisi hiyo. Baadhi ya nchi zimeondoka katika Mhakama hiyo, nyingine badozikifikiria kufanya hivyo ", rais Kenyatta amesisitiza.

"Tulitaka kufanya mabadiliko ambayo ingepelekea ICC kuheshimu uhuru wa taifa, lakini mabadiliko hayo hayakufanyika. Kwa hiyo tutathmini kwa kina juu ya uanachama wetu katika mkataba wa Roma unaounda Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu, " rais Uhuru Kenyatta ameongeza.

Tangu kuanzisha shughuli zake mwaka 2003, ICC imefungua uchunguzi kwa viza kumi, ikiwa ni pamoja nane kwa nchi za Afrika. Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto walistakiwa na ICC kwa madai ya kuhusika katika uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 hadi 2008. Lakini kesi dhidi yao ilifutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.