Pata taarifa kuu
KENYA

Walinzi 11 wa rais Kenyatta ni miongoni mwa watu walioangamia katika mkasa wa moto Kenya

Walinzi 11 wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa watu zaidi ya 30 walioangamia katika ajali ya moto Jumamosi usiku katika barabara ya Naivasha kwenda Nakuru.

Moja ya gari lililoteketea moto baada ya kutokea kwa mkasa wa moto
Moja ya gari lililoteketea moto baada ya kutokea kwa mkasa wa moto Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambirambi kwa jamaa ndugu na marafiki wa familia ya walinzi hao na watu wengine walioangamia katika mkasa huo uliojiri baada ya Lori kugonga magari mengine 13 yaliyoteketea moto.

Walinzi wa rais Kenyatta walikuwa wametoka katika Kaunti ya Bomet Magharibi Magharibi mwa nchi hiyo walikokuwa wamekwenda kutoa ulinzi kwa Kenyatta aliyekuwa na mkutano wa hadhara.

“Tumepoteza maafisa 11 wa GSU ambao ni walinzi wa rais Uhuru Kenyatta,” alisema Manoa Esipisu msemaji wa Ikulu.

Maafisa hao wa usalama kutoka kampuni ya G walikuwa wanasafiri wakitumia gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba GK B 961G wakirejea jijini Nairobi.

Polisi wanaendeleza kufanya uchunguzi kubaini chanzo hasa cha mkasa huo.

Kumekuwa na ripoti zinazokanganya ikiwa Lori hilo lilikuwa limebeba petroli au gundi.

Manusura wamekimbia kituo cha Televisheni KTN kuwa, lori hilo halikuwa la mafuta bali la gundi au kitu kama hicho ambacho kinashika moto kwa haraka.

Waziri wa Usalama wa ndani Joseph Nkaisery amesema, uchunguzi unaendelea kubaini ni kitu gani hasa kilichosababisha mkasa huo.

"Nawaomba wakenya wawe watulivu na baada ya uchunguzi kubainika, tutawaeleza kilichotokea," alisema.

"Tunawaomba Madereva na watumiaji wengine wa barabara kuwa makini kipindi hiki cha sikukuu."

Mkasa kama huo haujawahi kushuhudiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.