Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Benjamin Mkapa ziarani Burundi

Aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, akiwa pia msuluhishi kati ya Warundi anatazamiwa kuzuru nchi ya Burundi kuanzia Jumatano Desemba 7 hadi Ijumaa 9. Katika ziara hiyo Benjamin Mkapa atakutana na viongozi mbalimbali serikalini na mashirika ya kiraia.

Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania.
Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania. © MWANZO MILLINGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msuluhishi kati ya Warundi, Benjamnin Mkapa anafanya ziara nchini Burundi, wakati ambapo nchi hii bado inakabiliwa na mgogoro, huku mazungumzo yakiwa yamesimama kwa miezi kadhaa sasa.

Hata hivyo serikali ya Burundi iliapa kutokaa kwenye meza ya mazungumzo na makundi ya watu ambao inadai kuwa walihusika katika jaribio lililoshindwa la tarehe 13 hadi 14 Mei 2015.

Umoja wa Matiafa, Umoja wa Ulaya na Maekani wamekua wakiomba serikali ya Burundi kuanzisha haraka bila masharti mazungumzo na upinzani uliyokimbia uhamishoni kwa lengo la kudumisha usalama na kurejesha amani nchini mwake.

Hali ya usalama nchini Burundi imeendelea kutisha katika maeneo mbalimbali, hasa mjini Bujumbura, ambapo watu wamekua wakiokotwa maiti, huku visa vya utekaji nyara vikikithiri katika baadhi ya maeneo ya nchi ya Burundi.

Machafuko nchini Burundi yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 500 kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na zaidi ya laki mbili na elfu hamsini kuyahama makazi yao na kukimbilia nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.