Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Rwanda kuanza kuwachunguza maafisa wa Ufaransa kwa tuhma za kuhusika na mauaji ya Kimbari

Serikali ya Rwanda, imeanzisha uchunguzi dhidi ya maafisa 20 wa Ufaransa wanaoshukiwa kuchochea na kufadhili mauaji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi Mkuu wa mashtaka nchini humo Richard Muhumuza amesema, Rwanda imeshaifahamisha serikali ya Ufaransa kuhusu uchunguzi huu na inatumai itatoa ushirikiano.

Rwanda imeendelea kuishtumu Ufaransa kuwa ilitoa mafunzo kwa waliotekeleza mauaji hayo lakini pia kutochukua hatua yoyote kuyazuia, madai ambayo yameharibu uhusiano kati ya nchi hizi mbili tangu mwaka 1994.

Mauaji hayo ya kimbari yalisababisha vifo vya watu 800,000 wengi wao wakiwa ni kutoka kabila la Kitusti.

Kigali inasema hatua yoyote itakayochukuliwa baada ya uchunguzi huo kukamilika, itafahamika baadaye.

Rais Paul Kagame mwezi Oktoba mwaka huu alikasirishwa na uamuzi wa serikali ya Ufaransa kuanza kuchunguza upya kilichosababisha kuanguka kwa ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda kabla ya mauaji hayo ya Kimbari Juvénal Habyarimana.

Ufaransa imekuwa ikisema inataka kusikia ushahidi wa aliyekuwa Jenerali wa kijeshi wakati wa kipindi hicho cha mauaji ya kimbari Faustin Kayumba Nyamwasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.