Pata taarifa kuu
UNCHR-BURUNDI

UNHRC: Yaunda jopo la uchunguzu kuhusu Burundi licha ya pingamizi

Miezi miwili baada ya kutolewa kwa ripoti ya uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi unaofanywa na vyombo vya Serikali, umoja wa Mataifa umetangaza kuunda tume maalumu kuchunguza visa hivyo.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein.
Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein. UN Photo/Rick Bajornas
Matangazo ya kibiashara

Licha ya Serikali ya Burundi kupinga uundwaji wa tume hiyo na kuikana ripoti ya wataalamu wa umoja wa Mataifa, tume ya haki za binadamu ya umoja huo, imeendelea mbele na mpango wake, ambapo imetangaza wajumbe wa tume ya kuchunguza visa hivyo.

Jopo la wachunguzi huru wa umoja wa Mataifa, walianisha kwenye ripoti yao uwezekano wa kuwa vyombo vya usalama nchini humo huenda vikawa vimetekeleza makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu toka kuzuka kwa machafuko ya kisiasa baada tu ya mwezi April mwaka 2015.

Hata hivyo katika kile kinachoonekana ni dhamira ya tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa kutaka kuwashughulikia waliohusika kwenye visa hivyo, imeamua kuunda tume hiyo chini ya azimio namba 33/24 lililoridhiwa na baraza hilo, Septemba 30 mjini Geneva.

Tume hii mpya iliyoundwa, inahusisha watu mashuhuri ambao maisha yao yote wamekuwa wakipigania haki za binadamu.

Timu ya wachunguzi hao itaongozwa na Fatsah Ouguergouz kutoka Algeria ambaye anaijua Burundi vizuri kwakuwa aliwahi kuwa mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo.

Tume hii itakuwa na jukumu la kufanya uchunguzi wa kina na kuainisha ukweli halisi wa makosa yenyewe pamoja na kuwabaini wahusika wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ili wafikishwe mahakamani.

Hata hivyo jukumu la wachunguzi hawa huenda likawa gumu zaidi kwa kuwa tayari Serikali imeshatangaza kujitoa kwenye mahakama ya ICC na inapinga uchunguzi wowote unaotaka kufanywa dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.