Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wakimbizi wa Burundi wajaza makambi nchini Tanzania

media Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini Tanzania inayowapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wa Burundi Phil Moore/Oxfam

Kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania, zinakaribia kuzidiwa na uwezo wa kuwapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wanaoendelea kuingia nchini humo karibu kila siku.

Shirika la Kimataifa la Madktari wasiokuwa na mipaka la MSF linasema hali hii ni hatari na huenda hali ikawa mbaya zaidi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.

MSF inasema kati ya wakimbizi Laki tatu waliokimbia Burundi, zaidi ya laki mbili wanaishi nchini Tanzania katika kambi ya Nyarugusu.

Idadi hii ya wakimbizi waliofurika katika kambi hiyo inatishia kulipuka kwa magonjwa kama kipindupindu kutokana na maji safi ya kunywa, ukosefu wa chakula na hata maswala ya usalama.

Laurent Ligozat Naibu Mkurugenzi wa MSF kuhusu wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania 21/11/2016 Kusikiliza

Akizungumza na RFI, Naibu Mkurugenzi wa MSF Laurent Ligozat amesema hali hii ikiendelea kama inavyoshuhudiwa, idadi kubwa ya wakimbizi hao hasa watoto na wanawake watakuwa katika hali mbaya ya kiafya.

“Tumeshuhudia ongezeko la wakimbizi likiongezka mara tano katika miezi ya hivi karibuni, na tunahofia hali yao ya kiafya na usalama katika siku zijazo,” ameiambia RFI.

Mama akiwa na mtoto katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu nchini Tanzania Phil Moore/Oxfam

Nalo Shirika la Kimataifa la kutoa misaada ya kibinadamu la Oxfam, katika siku za hivi karibuni limetoa onyo kama hili.

Oxfam imeendelea kuwasaidia wakimbizi hao tangu mwaka 2015 kwa kuwapa maji safi ya kunywa, chakula, mahema na kuwachimbia vyoo na maeneo ya kutupa taka.

Serikali ya Burundi katika hatua nyingine imekuwa ikisema kuwa, hali ya usalama imesharejea nchini humo na kuwataka raia wake kurudi nyumbani.
 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana