Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye akamatwa na polisi kwa mara nyingine

media Kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye akisindikizwa na maofisa wa gereza la Luzira alikokuwa akishikiliwa DR

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Daktari Kizza Besigye amekamatwa na polisi jumamosi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kasangati wilayani Wakiso.

Muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake Dr Besigye,kama kawaida alirushiana maneno na mkuu wa polisi wa kituo cha Kasangati Bwana Robert Kachumu.

Daktari kizza Besigye alikamatwa baada ya kutomjibu afisa huyo wa polisi ambaye alitaka kujua Kizza Besigye anaenda wapi.

Kwa mujibu wa Daily Monitor la nchini Uganda Kizza Besigye alijitetea kuwa ana haki ya kutembea kama raia wengine.

Besigye analaani kuzuiwa nyumbani na uwepo wa askari wengi kuzunguka makazi yake.

Besigye ambaye alikuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha FDC alikamatwa masaa kadhaa baada ya kundi la wanachama wa upinzani kuwaambia waandishi wa habari kuwa wana mpango wa kuligawa bunge kufuatia kuzuiwa nyumbani kwa kiongozi huyo.

Inaelezwa kuwa Daktari Kizza Besigye anashikiliwa katika kituo cha polisi Nagalama wilayani Mukono.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana