Pata taarifa kuu
BURUNDI-ICC

ICC: uamuzi wa Burundi wa kujiondoa ICC si mwisho wa kutofunguliwa mashitaka

Nchini Burundi, yote yalienda kwa haraka mno baada ya serikali kuchukua uamuzi wa kujiondoa kama mwanachama wa Mahakama ya kimataifa ya Jinai (ICC), ikituhumiwa kuwa 'chombo cha kisiasa cha ukandamizaji.'

Fatou Bensouda wakati alipokua akila kiapo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini Hague tarehe 15 Juni 2012.
Fatou Bensouda wakati alipokua akila kiapo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini Hague tarehe 15 Juni 2012. AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Bunge, baraza la Seneti limepiga kura kwa uamuzi wa serikali ya Burundi wa kujiondoa kama mwanachama wa ICC na sasa ni zamu ya Rais Pierre Nkurunziza kutia saini. Itakua ni kwa mara ya kwanza kwa mahakama hiyo, lakini kwa uhakika, uamuzi huo hauitengi Burundi kutofunguliwa mashitaka mbele ya mahakama ya kimataifa.

Kimsingi, Mahakama ya Kimataifa haiwezi tena kuchunguza kwa jitihada zake nchini Burundi, mara tu mwaka mmoja utakua umemalizika baada ya nakala hiyo kutiliwa saini na rais wa Burundi. Hata hivyo uamuzi huo hautoitenga Burundi kutofuatiliwa na mahakama ya kimataifa. Inatosha tu kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuruhusu nchi hiyo kufuatiliwa na mahakama ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa kesi ya Darfur mwaka 2005 na Libya mwaka 2011.

Jumuiya ya kimataifa pia imeweka wazi kesi ya wanachama ambao wataamua kujiondoa katika ICC ili kuepuka mashtaka, mtaalamu aliyehojiwa na RFI ameeleza. Sheria za Roma zinaeleza kwamba 'uamuzi wa kujiondoa ICC unachukua mwaka mmoja baada ya tarehe ambayo uamuzi huo utakua umewasilishwa kwa vyombo husika,' uamuzi wa kujiondoa hautakua na athari kwa kesi ambazo tayari zinaendelea kushughulikia na taasisi hiyo ya kimataifa hata kama uamuzi huo utasahihishwa.

Mwendesha mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda, alizindua mwezi April mwaka huu uchunguzi wa awali kuhusu mauaji, mateso na ubakaji nchini Burundi. Wakati huo huo, kundi la wanasheria liliwasilisha kwa Mahakam ya Kimataifa ya Jinai (ICC) tangu miezi mitatu iliyopita kesi ya waathirika zaidi ya mia moja au warithi wa waathirika wa unyanyasaji huo.

Hatimaye, na hii pengine ni moja ya sababu iliyopelekea serikali ya Burundi kuchukua uamuzi wa kujiondoa katika ICC: baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa liliamua, siku chache tu zilizopita kuunda tume ya uchunguzi wa kimataifa kufuatia ripoti ya wataalam iliyohusisha serikali ya Burundi katika uhalifu mkubwa. Orodha ya wahusika katika uhalifu huo tayari imewekwa wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.