Pata taarifa kuu
DADAAB-KENYA-SOMALIA

Mashirika ya kibinadamu yakosoa urejeshwaji wa wakimbizi wa Somalia

Shirika moja la misaada la Kimataifa, linasema kuwa nchi ya Kenya inakiuka sheria za kimataifa kwa kuwalazimisha kurudi nyumbani kwa nguvu wakimbizi wa Somalia, wanaohifadhiwa kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Dadaab.

Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari.
Sehemu ya wakimbizi wa Somalia walioa kurejea nyumbani kwa hiari. unchr.org
Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Kenya yenyewe inasema kuwa, zoezi la kuifunga kambi ya Dadaab, inayowahifadhi maelfu ya raia wa Somalia, linafanyika kwa misingi ya haki na kufuata sheria za kimataifa, lakini shirika la misaada la nchini Norway NRC, limesema kuwa zoezi hilo halikizi sheria za kimataifa.

Hatua hii inamaanisha kuwa nchi ya Kenya huenda ikakutwa na hatia chini ya sheria za kimataifa kwa kuwalizimisha kwa nguvu kurudi nyumbani kwa wakimbizi na waomba hifadhi.

“Shinikizo kuwalazimisha zaidi ya wakimbizi elfu 28 waliosajiliwa kutoka kambi ya Dadaab, kumewaweka kwenye mazingira magumu.” limesema shirika la NRC.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Jan Egeland amesema kuwa “kutokana na kile tulichokiona, zoezi hili sio tena la kurejea nyumbani kwa hiari, salama wala la utu.”

Serikali ya Kenya mwezi Mei mwaka huu ilitangaza kuwa itaifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab mwishoni mwa mwaka huu kutoka na kile inachosema ni kwa sababu za kiusalama ikiwatuhumu wakimbizi hao kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia.

NRC inasema kuwa kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao, kwenye taifa ambalo haliko salama kwa sasa, hakutoi hakikisho la ulinzi na usalama wa raia hao wanaorejea nyumbani kwa hiari huku huduma nyingi za kijamii zikikosekana kwenye maeneo walikotoka.

Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi duniani, UNHCR, linatuhumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu, kwa kukubali na kuwa sehemu ya mpango wa Serikali kuwarudisha kwa nguvu maelfu ya wakimbizi kutoka kwenye kambi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.