Pata taarifa kuu
KENYA-DINI

Mjane wa Sheikh Aboud Rogo aachiliwa huru kwa dhamana

Mahakama mjini Mombasa nchini Kenya imemwachilia kwa dhamana Hania Said Sagaar, Mjane wa mhubiri aliyeuawa mwaka 2012 Sheik Aboud Rogo, aliyeuawa kwa madai ya kutoa mafunzo ya Itikadi kali.

Hania Said Sagaar, Mjane wa mhubiri aliyeuawa mwaka 2012 Sheik Aboud Rogo, aliyeuawa kwa madai ya kutoa mafunzo ya Itikadi kali.
Hania Said Sagaar, Mjane wa mhubiri aliyeuawa mwaka 2012 Sheik Aboud Rogo, aliyeuawa kwa madai ya kutoa mafunzo ya Itikadi kali. NATION MEDIA GROUP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Shanzu licha ya kumpa dhamana, imemuagiza Sagaar awe anaripoti mara moja kila mwezi katika kituo cha Polisi cha Nyali.

Aidha Mahakama hiyo imesema mama huyo wa watoto 7 kutokana na majukumu makubwa ya kifamilia inafahamu kuwa itakuwa vigumu kwake kukwepa Mahakama.

Anahusika kwa kushirikiana na wanawake watatu walioshambulia kituo cha polisi mwezi huu, na kubainika kuwa aliwasiliana kwa simu na mmoja wa washukiwa hao aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Mji wa Mombasa umekuwa ukilengwa na kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka mjini Somalia, baada ya kutuma jeshi lake nchini humo mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.