Pata taarifa kuu
TANZANIA

Tanzania yazindua ndege mbili za abiria ilizonunua kutoka Canada

Tanzania imezindua ndege mbili za usafiri wa angaa aina ya Q 400 kutoka kwa kampuni ya ndege ya Bombardier kutoka nchini Canada.

Ndege mbili za Tanzania zilizozinduliwa na rais John Magufuli Septemba 28 2016
Ndege mbili za Tanzania zilizozinduliwa na rais John Magufuli Septemba 28 2016 Issa Michuzi
Matangazo ya kibiashara

Ndege hizo mbili zina uwezo wa kuwabeba abiria 76, na zitatumiwa kuwasafirisha abiria ndani ya nchi hiyo na  nchi jirani.

Akizindua ndege hizo, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, rais John Pombe Magufuli amesema usafiri wa ndege hizo, utasaidia kufufua Shirika la ndege nchini humo la ATCL.

Tanzania ambayo ni nchi kubwa katika eneo la Afrika Mashariki, imekuwa ikitatizika katika safari za angaa na kuwalazimu abiria kutumia ndege za kibinafsi kufika miji mbalimbali.

Aidha, ndege hizi zinatarajiwa kuwasafirisha watalii kufika katika vituo mbalimbali vya utalii.

Rais Magufuli amewataka raia wa nchi hiyo hasa wafanyikazi wa serikali kutumia usafiri wa ndege hizi mpya ili kuimarisha Shirika hilo la ndege.

Aidha, ameongeza kuwa serikali yake inapanga kununua ndege zingine mbili zitakazokuwa na uwezo wa kuwabeba abiria zaidi ya 100 katika siku zijazo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi barani Afrika ambayo imefanikiwa kununua ndege kutoka Shirika la ndege la Bombardier.

Kampuni hiyo imefanikiwa kuuza zaidi ya ndege 160 katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.