Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Afisa mtoro atangaza vita dhidi ya serikali ya Salva Kiir

Mmoja wa viongozi wa kijeshi nchini Sudan Kusini, ametangaza kuunda kundi lake la uasi kupambana na serikali ya Juba, siku mbili baada ya aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar kutangaza vita dhidi ya serikali ya rais Salva Kiir.

Jeshi la Uganda katika msafara wa kijeshi likielekea Juba, Julai 14, 2016.
Jeshi la Uganda katika msafara wa kijeshi likielekea Juba, Julai 14, 2016. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la waasi linaongozwa na aliyekuwa wakati mmoja mwanajeshi katika jeshi la serikali ya Sudan Kusini na ambaye ametoroka jeshini, luteni Jenerali Khalid Boutros Bora.

Jenerali huyo alitoa tangazo hilo mahali ambapo hakutaka patajwe kwa ajili ya usalama wake nchini sudan Kusini na anasema kuwa yuko tayari kuungana na wapiganaji wengine kuiangusha serikali ya rais Salva Kiir.

“Kundi la kijeshi la chama cha kisiasa cha upinzani cha kisiasa cha South Sudan Democratic Movment, (SSDM), linatangaza kuwa kuanzia sasa linaazisha vita vikali vya kijeshi dhidi ya serikali ya kidhalimu, na ya kikabila ya Juba. Ikitiliwa maanani kuwa kuna haja kuimarisha upinzani dhidi ya serikali ya Juba, kundi la kijeshi la SSDM ambalo kitengo chake cha kijeshi kinajulikana kama COBRA, kinaanzisha mapambano ya ushirikiano na makundi mengine ya upinzani ya kijeshi ambayo tayari yako katika uwanja wa mapambano, “ amesema luteni Jenerali Khalid Boutros Bora.

Mpaka sasa serikali ya Juba haijatoa matamshi yoyote kumhusu Jenerali huyo muasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.