Pata taarifa kuu
UGANDA

Besigye apangiwa makaribisho makubwa, polisi wasema hawafahamu

Polisi nchini Uganda wanasema hawajapata taarifa zozote za kuwepo kwa maandamano ya kumpokea kiongozi wa upinzani Kizza Besigye anayetarajiwa kurejea nchini humo siku ya Alhamisi akitokea nchini Uingereza na Marekani.

Kizza Besigye kiongozi wa upinzani nchini Uganda
Kizza Besigye kiongozi wa upinzani nchini Uganda RFI/Charlotte Cosset
Matangazo ya kibiashara

Besigye amekuwa ziarani katika mataifa hayo kwa wiki tatu sasa.

Chama cha FDC kimewataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kumkaribisha kiongozi wao, na kuandamana naye kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe hadi jijini Kampala.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini humo Andrew Kawesi amesema, jeshi hilo lilisikia taarifa za kuwepo kwa maandamano ya kumkaribisha kiongozi huyo, kupitia vyombo vya Habari.

Hata hivyo, mmoja wa wanasiasa wa chama cha FDC Wafula Ogutu amesema tayari wamewaambia polisi harakati zao za kumpokea kiongozi wao.

Besigye ambaye aliwania urais nchini mwake na kudai kuwa aliibiwa kura na rais Yoweri Museveni, ametumia ziara zake nchini Marekani na Uganda kutoa mihadhara kuhusu hali ya kisiasa nchini mwake na harakati zake za kushinikiza mabadiliko.

Mahakama jijini Kampala ilimpa ruhusa ya kusafiri nje ya nchi kwa sababu anakabiliwa na kesi ya uhaini baada ya kujiapisha kama rais wa Uganda baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Februari.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.