Pata taarifa kuu
ICJ-KENYA-SOMALIA

Somalia yaijia juu Kenya kuhusu eneo la bahari wanaloliwania

Nchi ya Somalia inaituhumu Serikali ya Kenya, kuendeleza mvutano usio wa lazima kuhusu eneo la bahari ya Hindi linalowaniwa na nchi hizo mbili katika mahakama ya usuluhishi wa mipaka, ICJ, ambapo Somalia inasema suala hilo lilikuwa na uwezo wa kutatuliwa kwa kutumia busara kwa kuwa nchi zote mbili zina maslahi.

Majaji wa mahakama ya umoja wa Mataifa ya usuluhishi wa mipaka ICJ, mahakama hii ndio inasikiliza mzozo kati ya Kenya na Somalia
Majaji wa mahakama ya umoja wa Mataifa ya usuluhishi wa mipaka ICJ, mahakama hii ndio inasikiliza mzozo kati ya Kenya na Somalia RFI/Dyna Seng
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Mogadishu pia, umekashifu tuhuma zilizotolewa Jumatatu ya wiki hii na Serikali ya Kenya, ambayo ilieleza kusikitishwa na hatua ya nchi ya Somalia kuamua kulipeleka suala hilo kwenye mahakama ya ICJ, hatua ambayo Kenya inasema ni kuchochea mzozo uliopo.

Wakili wa nchik ya Somalia kwenye kesi hiyo, Mona al-Sharmani, ameiambia mahakama kuwa “hatutaki zaidi wala hatutaki pungufu yake, zaidi tunataka mzozo kati yetu na kaka zetuj na dada zetu wa Kenya, upate suluhu ya kudumu kwa njia iliyo bora,” alisema wakili huyo.

Wakili Mona ameongeza kuwa, Somalia iliamua kugeukia mahakama ya ICJ baada ya miaka mingi ya ugumu na wakati fulani kutoleana maneno makali na ndugu zao wa Kenya kwenye majadiliano ambayo hata hivyo yameonesha kushindikana.

Mvutano mkubwa uliopo wa kisheria baina ya nchi hizi mbili ni kuhusu namna ambavyol mpaka mpya utachorwa.

Nchi zote mbili zinadai kuwa na umiliki wa eneo la pembe tatu la bahari ya hindi ambalo lina ukubwa wa kilometa laki moja za mraba na lina aminika kuwa na utajiri mkubwa wa hifadhi ya mafuta na gesi.

Somalia ambayo inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini, inataka mpaka wake uliozitenganisha nchik hizo mbili, utumike kupima eneo linalowaniwa, lakinik Kenya yenyewe inataka uchorwe mstari mnyoofu kutoka kwenye pwani yake.

Nchi ya Somalia ilifungua shauri hili katika mahakama ya ICJ mwaka 2014, na inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo lakini kwa sasa inajadili ikiwa mahakama hiyo ya umoja wa Mataifa ina mamlaka kusikiliza shauri hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.