Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Wadau wa siasa Tanzania wapongeza hatua ya upinzani kuahirisha maandamano

Wadau wa siasa na viongozi wa dini nchini Tanzania, wamepongeza uamuzi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kutangaza kuahirisha kufanyika kwa maandamano ya nchi nzima waliyokuwa wamepanga yafanyike September Mosi mwaka huu.

Bendera za chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema
Bendera za chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema wantedinafrica.com
Matangazo ya kibiashara

Jumatano ya Agosti 31, mwenyekiti taifa wa chama cha CHADEMA, Freeman Haikeli Mbowe alitangaza kuwa, kamati ya uongozi ya chama hicho imekubaliana kwa kauli moja kusogeza mbele maandamano yao hadi October Mosi, kupisha mchakato wa kusaka suluhu ulioanzishwa na viongozi wa dini.

Mbowe amesema kuwa uamuzi wao umetokana na kuombwa na viongozi wa dini kuinusuru nchi kutumbukia kwenye vurugu ambazo zingeweza kuepukika na ndio maana wakaamua kuwasikiliza viongozi wa dini.

Chama hicho kimesema muda kiliotoa ni kutoa fursa kwa Serikali kufikiria upya uamuzi wake wa kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa.

Wadau wa siasa walioongea na idhaa hii wameeleza kuridhishwa na uamuzi wa Chadema kuamua kuachana na azma yao ya awali, wakisema kuwa ni utashi wa kisiasa walioutumia kwa kuangalia maslahi ya taifa.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, walitarajia kuona chama hicho kikichukua maamuzi ya kuahirisha maandamano yao, kutokana na hali ya sintofahamu iliyokuwa imetanda nchi nzima kwa hofu ya kutokea kwa vurugu.

Viongozi wa dini kwa upande wao wamepongeza uamuzi wa upinzani kuahirisha maandamano hayo na kuongeza kuwa wanafanya kila linalowezekana wakutane na rais pamoja na wadau wengine katika kuzungumzia mustakabali wa siasa za Tanzania ili kunusuru kutokea kwa kile kilichokuwa kikihofiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.