Pata taarifa kuu
TANZANIA

Wadau wa habari Tanzania watoa maoni baada ya kufungiwa kwa vyombo vya habari

Siku moja baada ya kufungiwa kwa muda kwa vyombo viwili vya habari, Radio Five ya mkoani Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaa, wadau wa habari wamekuwa na maoni tofauti kuhusu uamuzi uliotangazwa na Serikali.

Waziri wa habari nchini Tanzania, Nape Nnauye, akizungumza jijini Dar es Salaam, Tanzania, 29 agosti, 2016
Waziri wa habari nchini Tanzania, Nape Nnauye, akizungumza jijini Dar es Salaam, Tanzania, 29 agosti, 2016 RFI
Matangazo ya kibiashara

Akitangaza uamuzi huo Jumatatu ya wiki hii jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amesema amefikia uamuzi huo baada ya kujirdhisha kuwa kipindi vipindi vilivyorushwa na vituo hivyo kati ya Agosti 25 na Agosti 17 mwaka huu vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani.

Waziri Nape amesema kuwa amevifungia kwa muda usiojulikana vituo hivyo kwa kukiuka masharti na kanuni ya  5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na
c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Wakati vyombo hivyo vya habari vikifungiwa, baadhi ya wadau wa habari walioongea na idhaa hii wamekuwa na mtazamo tofauti, huku baadhi wakiunga mkono kwa kile wanachosema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, vipindi vingi vya redio vimekuwa havina maudhui chanya yenye kuleta chachu ya mabadiliko kwa jamii, na badala yake vimekuwa vikihamasisha mgawanyiko na kutengeneza chuki.

Wadai hao wameenda mbali zaidi na kudai kuwa umefika wakati, taaluma ya uanahabari ichukuliwe kwa umakini mkubwa hasa na wamiliki wa vyombo hivyo kwa kuhakikisha kuwa watangazaji wao wanazingatia maudhui mazuri ya vipindi vyao ili kuepusha kupotosha uma ama kutengeneza mazingira ya uchochezi.

Wapo pia wadau ambao wanapinga uamuzi huu wa Serikali kwa kile wanachosema kuwa vyombo vya habari viko huru katika kutoa mitazamo ya kile ambacho kimejiri katika jamii, ama kiwe na muonekano hasi au chanya isipokuwa wazungumzaji wake wamezingatia weledi kwa kuzungumza kile ambacho kimezungumza na kujadiliwa.

Wadau hao wametolea mfano vipindi vya hivi karibuni vilivyowahi kurushwa kwenye runinga na redio kukosa maadili huku kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano ikivifumbia macho vipindi hivyo ambavyo vilichukiza watu wengi na hata kuzua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri Nape, akatumia furas ahiyo kuvionya vyombo vingine vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda taaluma hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.