Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Viongozi wakuu wa chama cha Chadema wakamatwa Tanzania

Viongozi wakuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema wamekamatwa na polisi Jumatatu hii na kupelekwa katika kituo cha polisi mjini Dar es Salaam kwa mahojiano. Hali hii inatokea mwaka mmoja baada ya rais John  Pombe Magufuli kuchaguliwa kuliongoza taifa la Tanzania

Edward Lowassa, waziri Mkuu wa zamani, mmoja wa viongozi wakuu wa chama cha Chadema waliokamatwa, katika kampeni ya uchaguzi wa urais mjini Kilosa, katika mkoa wa Morogoro, Oktoba 23, 2015.
Edward Lowassa, waziri Mkuu wa zamani, mmoja wa viongozi wakuu wa chama cha Chadema waliokamatwa, katika kampeni ya uchaguzi wa urais mjini Kilosa, katika mkoa wa Morogoro, Oktoba 23, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mwanasheria wa chama cha Chadema, Tundu Lissu, amethibitisha kukamatwa kwa viongozi hao, akisem akuwa waliokamatwa ni pamoja na Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Vincent Mashinji na Saidi Issa.

Bw Lissu amesema viongozi hao walikamatwa wakiwa katika kikao cha kamati Kuu ya chma cha Chadema, kikao ambacho walihudhuria wabunge kwa minajili ya masuala mbalimbali ya chama hicho. Kikao hicho kilikua kimehudhuriwa na wajumbe 170.

Haijulikani ni sababu ipi ilisababisha maaafisa hao kukamatwa. Lakini inasema kuwa huenda watu hao walikamatwa kwa sababu wamekiuka agizo la kupiga marufuku mikutano.

Chama cha Chadema kinapanga kufanya mikutano ya nchi nzima Alhamisi wiki hii kupinga kile ilichokitaja kuwa ni kuingiliwa kwa haki ya kujieleza na demokrasia nchini Tanzania tangu rais John Pombe Magufuli kuingia madarakani mwaka uliopita.

Itafahamika kwamba Edward Lowassa aligombea katika uchaguzi wa urais uliyofanyika mwaka uliyopita, akishindana na rais John Magufuli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.