Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Sudani kusini yataka bajeti kubwa 2016-2017 licha ya kuzorota kwa uchumi

Serikali ya Sudani Kusini ambayo uchumi wake umezorota kufuatia miaka kadhaa ya vita imetaka kiwango kikubwa cha bajeti ya mwaka 2016-2017 ya takribani dola bilioni moja,kiwango kikubwa mara tatu zaidi ya mwaka uliopita.

Raisi wa Sudani kusini Salva Kiir
Raisi wa Sudani kusini Salva Kiir Charles Atiki Lomodong / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa habari wa sudani kusini Michael Makuei ameiambia AFP kuwa kusudi la bajeti hii ni kutekeleza makubaliano ya amani akirejelea mkataba uliosainiwa August 2015.

Pendekezo la bajeti hiyo halijaidhinishwa na bunge lakini huenda likaungwa mkono na wabunge wengi wa taifa hilo changa duniani hususan wanaotii serikali ya raisi Salva Kiir.

Hata hivyo bado haijafahamika taifa hilo litazipata wapi fedha hizo za bajeti wakati mapigano yakiendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi na kusababisha njia kuu za kiuchumi kuingia jiji kuu kufungwa.

Baada ya kuulizwa kuhusu wapi fedha hizo zitapatikana waziri wa habari alijibu kuwa wanajua watakapo pata fedha na kuongeza kuwa bajeti hiyo nikubwa zaidi ya mwaka jana kwa sababu mwaka jana hakukuwa na makubaliano

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.