Pata taarifa kuu
KENYA

Mkutano wa kibiashara kati ya Afrika na Japan wafunguliwa Nairobi leo

Mkutano wakimataifa wa biashara kati ya bara la Afrika na nchi ya Japan unaanza rasmi leo Jumamosi jijini Nairobi nchini Kenya. 

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akiwa na naibu wa rais wa Kenya  William Ruto,26 Agost 2016 jijini Nairobi.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akiwa na naibu wa rais wa Kenya William Ruto,26 Agost 2016 jijini Nairobi. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo maarufu kama TICAD unaofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika utadumu kwa siku mbili na unahudhuriwa na marais thelathini na watano pamoja na washiriki zaidi ya elfu kumi kutoka kote ulimwenguni.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe anatarajiwa kutumia mkutano huu kukutana na viongozi kutoka kote Afrika na kuweka wazi miradi ya misaada na uwekezaji ikiwa ni pamoja na miradi ya huduma za afya.

Akizungumza katika usiku wa mkutano huo, rais Uhuru Kenyatta amesema lengo la mkutano huo ni itakuwa kuangazia maendeleo ya viwanda, afya na utulivu.

Rais Kenyatta amesema mataifa mengi ambayo yameepuka umasikini kwa kukuza viwanda hivyo Afrika ina haja ya kuamka kwani maendeleo hayatatokea Afrika ikiwa waafrika hawatatumia fursa kufanya maendeleo.

Waziri mkuu Abe ameahidi kwamba Teknolojia bora ya Japan na maendeleo ya rasilimali watu vitasaidia sekta ya viwanda, ikiwa ni pamoja na katika kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.