Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

UNSC kupiga kura kuamua hatma ya wanajeshi elfu 4 kupelekwa Sudan Kusini

media Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa wakiwa kwenue moja ya mikutano yao hivi karibuni UN Photo/Manuel Elias

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa linapiga kura Ijumaa, Agosti 12, kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi elfu 4 wa kikosi maalumu nchini Sudan Kusini, licha ya upinzani toka kwa Serikali ya Juba.

 

Marekani ndiyo iliyowasilisha pendekezo hilo juma hili, na kulitaka baraza la usalama kutuma kikosi cha wanajeshi watakaokuwa na jukumu la kutoa usalama mjini Juba na kulinda kambi na ofisi zake nchini humo.

Mjadala mkali uliendelea ndani ya baraza la usalama hadi Alhamisi ya wiki hii, ambapo nchi za Urusi, China na Misri, zilieleza wasiwasi wao wa kutumwa kwa kikosi hicho cha wanajeshi elfu 4 bila kupata baraka za Serikali ya Juba.

Haya yanajiri baada ya juma hili, Serikali ya Juba, kudai kuwa haitakubali kupelekwa kwa wanajeshi wa ziada elfu 4 mjini Juba, kwa kile inachosema kufanya hivyo, ni kuingilia mamla na uhuru wa kujitawala wa taifa hilo.

Mji wa Juba ulishuhudiwa mapigano makali kwa siku kadhaa toka mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu, kati ya vikosi vya Serikali ya Rais Salva Kiir na vile vya aliyekuwa makamu wa Rais, Riek Machar.

Siku chache tu baada ya wakuu wa nchi za IGAD kukubaliana kutuma kikosi maalumu kitakachokuwa na mamlaka kama kile kilichopelekwa DRC, Serikali ya Juba ilikikubali, lakini Jumatano ya wiki hii, ikabadili msimamo wake.

Pendekezo hili la Marekani linataka nchi hiyo iwekewe vikwazo vya silaha ikiwa itaendelea kupinga kupelekwa kwa kikosi hicho, huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa suala hilo huenda likawa gumu.

Tume ya UNMISS iliyoko nchini Sudan Kusini chini ya umoja wa Mataifa, inalaumiwa kwa kushindwa kuwalinda rais na mali zao, huku kukiwa na ripoti za kukithiri kwa vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan Kusini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana