Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Tume ya uchunguzi ya UN yabaini sababu za UNMISS kushindwa kudhibiti mgogoro wa Sudan Kusini

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa UN imebaini kuwa walinda amani wa umoja huo nchini Sudan Kusini  UNMISS walishindwa kumudu kikamilifu mgogoro wa Sudan Kusini baada ya kambi yao kushambuliwa vikali miezi sita iliyopita.

Raia wa Sudan Kusini wakikimbia mapigano baada ya mtu kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Malakal Februari 18 2016
Raia wa Sudan Kusini wakikimbia mapigano baada ya mtu kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Malakal Februari 18 2016 Justin LYNCH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bodi ya tume hiyo iliyoundwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon imetoa ripoti yake na kusema kuwa walinda amani hao waliondoka katika kambi yao ya Malakal baada ya kushambuliwa mnamo Februari 17 na 18.

Karibu watu 30 waliokuwa wanahifadhiwa katika kambi ya Malakal waliuawa katika vurugu hizo na 123 walijeruhiwa.

Aidha bodi hiyo imesema kuwa kuna mkusanyiko wa sababu ambazo zilichangia vurugu ikiwa ni pamoja na mvutano kati ya makundi ya kikabila ya Shilluk, Dinka na Nuer ambao wanafanya jumla ya watu elfu 48 wanaoishi katika kambi ya Malakal.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.