Pata taarifa kuu
UNSC-BURUNDI

UNSC yapiga kura ya kupeleka askari polisi 228 Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloruhusu kupelekwa kwa askari polisi 228 nchini Burundi. Nchi hii imeendelea kukumbwa na machafuko, baada tu ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania urais kwa muhula wa tatu, uamuzia ambo alifikia, na kuchaguliwa mwezi agosti mwaka 2015. Uchaguzi ambo upinzani ulisusia

RAis wa Burundi Pierre Nkurunziza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, Februari 23, 2016 Bujumbura.
RAis wa Burundi Pierre Nkurunziza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, Februari 23, 2016 Bujumbura. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ilikuwa katika harakati kwa miezi kadhaa ili kupelekea kuwepo ujumbe wa kimataifa katika nchi hii ambapo baadhi ya wanachama wa jumuiya ya kimataifa wana hofu ya kutokea kwa mauaji ya kimbari. Lakini mgawanyiko ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaonyesha kwamba vikwazo vingi bado vipo kabla ya kikosi hiki cha polisi ya Umoja wa Mataifa kuingia nchini Burundi.

Ufaransa imeonekana kupata ushindi mdogo wa kidiplomasia Ufaransa, ambapo imepata kura 11 katika neema ya kupelekwa kwa kikosi cha polisi kwa muda wa mwaka mmoja nchini Burundi.

Hata hivyo Ufaransa bado haijapata ushindi kamili, kwani itachukua wiki ya mazungumzo ili kupata idhini ya Urusi na uhakika kwa China kwamba haitopinga azimio hilo kwa kura yake ya turufu. Nchi hizi mbili bado zinatetea na kuzingatia uhuru wa taifa la Burundi.

Na upande mwengine Misri, Angola na Venezuela zilijizuia kupiga kura zikibaini kwamba kuna haja ya kupata idhini kutoka serikali ya Burundi ambayo imekua ikisisitiza kupelekwa kwa askari polisi 50 pekee.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua hiyo akisema ni kuwa " kitendo hicho ni muhimu kwa kuzuia mauaji ya kimbari ambayo yanaweza kutokea" katika nchi hiyo ndogo ya Afrika Mashariki. Akizungumzia mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, François Delattre amebaini kupitishwa kwa azimio hili, kunaonyesha jinsi gani Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "limejifunza kwa yale yaliyotokea zamani."

Eneo kulikotokea shambulizi la guruneti Bujumbura, Burundi, Februari 15,2016.
Eneo kulikotokea shambulizi la guruneti Bujumbura, Burundi, Februari 15,2016. STRINGER / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.