Pata taarifa kuu
KENYA

Watumiaji wa dawa za kulevya wana hatari zaidi kuambukizwa UKIMWI

Wadau wa mashirika ya kupambana na matumizi ya mihadarati nchini Kenya, wanasema idadi kubwa ya waraibu wa mihadarati wanaishi na virusi vinavyo sababisha UKIMWI.

Mmoja wa watumiaji wa dawa za kulevya, akionekana anajidunga sindano ya dawa hizi.
Mmoja wa watumiaji wa dawa za kulevya, akionekana anajidunga sindano ya dawa hizi. DR
Matangazo ya kibiashara

Afisa mkuu wa kituo cha kutoa ushauri kwa waraibu wa mihadarati cha Reach Out Center mjini Mombasa, Taib Abdulrahaman, anasema asilimia 18 ya watu wanaotumia mihadarati wanaishi na virusi vya ukimwi.

Abdhulrahamani amasema takwimu hizo zinatia hofu na sasa wanapanga mikakati ya kutoa hamasa kwa waraibu wa mihadarati katika maeneo tofauti ukanda wa pwani ili kukabiliana na tatizo hilo.

Taib anasema mpango wa serikali wa kupeana sindano miongoni kwa waraibu wa mihadarati wanaojibwenga, umesaidia pakubwa kupunguza maambukizi ya maradhi tofauti.

RFI Kiswahili imezungumza na mmoja wa waraibu wa mihadarati mjini Mombasa nchini Kenya kuhusiana na mpango huo wa serikali, ambapo wamesema bado hawahudumiwi ipasavyo na Serikali kutoka kwenye hali waliyo nayo.

Idara ya usalama ukanda wa pwani hapa nchini Kenya imekuwa ikiendelea na opareshemi kali za kuwasaka walanguzi wakuu wa mihadarati ambao wanatajwa kuathiri vijana wengi.

Waraibu hao wanasema wanalazimika kufanya vitendo visivyo vya kaida na hatari kwa maisha yao, huko wakiomba hatua za harata kuchukuliwa ili kuwanusuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.