Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Rwanda yasema haita mkamata Rais Bashir licha ya Waranti ya ICC

media Louise Mushikiwabo, waziri wa mambo ya nje wa Rwanda. AFP PHOTO/ TONY KARUMBA

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, amekaribishwa na Serikali ya Rwanda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, unaonza mwishoni mwa juma hili jijini Kigali.

tangazo hili limetolewa na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, ambaye ametupilia mbali ombi la mahakama ya ICC, iliyotuma kwa nchi yake siku mbili zilizopita wakitaka utawala wa Kigale umkamate Rais Bashir atakapowasili nchini humo.

Akizungumza na wanahabari jijini Kigali, waziri Mushikiwabo, amewaambia waandishi wa habari kuwa, Serikali yao kwasasa iko bize na masuala mengine ya kitaifa na kwamba haina muda wa kutazama suala hilo.

"Rwanda ni mwenyeji wa wakuu wa nchi walioalikwa na umoja wa Afrika," alisema waziri Mushikiwabo.

"Na kwa mantiki hiyohiyo, kila mtu aliyealikwa na umoja wa Afrika, ataruhusiwa kuingia Rwanda na kukaribishwa kama wageni wengine, na kwamba atakuwa chini ya ulinzi wa Serikali ya Rwanda ikiwa kuna jambo lolote litataka kufanywa," alimaliza waziri Mushikiwabo.

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anayesakwa na mahakama ya ICC REUTERS/Siphiwe Sibeko

Mahakama ya kimataifa ya OCC, ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa rais Bashir mwaka 2009 na 2010 akihitajika kwa makosa ya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, na mauaji ya halaiki, uhalifu anaodaiwa kuutekeleza kwenye jimbo la Darfur, ambako watu zaidi ya laki 3 wamekufa, kwa mujibu wa umoja wa Mataifa.

Hata hivyo licha ya kutolewa kwa hati hiyo, Rais Bashir ameendelea kusafiri katika baadhi ya nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa mahakama ya ICC bila kumkamata.

Hali ilikuwa ni ya kukanganya mwaka uliopita, wakati Serikali ya Afrika Kusini iliposhindwa kumkamata Rais Bashir, alipohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, AU, jijini Johannesburg.

Viongozi wa Afrika, hata hivyo wameendelea kuweka shinikizo na pingamizi kuhusu mahakama hiyo, wakiituhumu kuwalenga baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika.

Waziri Mushikiwabo amethibitisha kuwa, kutakuwa na mjadala siku ya Jumapili na Jumatatu wakati wa kufungwa kwa mkutano huo, kujadili ikiwa nchi za Afrika zijiondoe kwenye mkataba wa Roma.

Mwaliko huu umekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita, toka mahakama ya ICC itangaze kuzipeleka nchi za Uganda na Djibouti, kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa, baada ya nchi hizo kushindwa kwa makusudi kumkamata Rais Bashir mwezi May.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana