Pata taarifa kuu
BURUNDI-BENJAMIN MKAPA-MAZUNGUMZO

Burundi: raundi ya pili ya mazungumzo ya kumaliza mgogoro Arusha

Mazungumzo juu ya mustakabali wa Burundi yanaanza Jumanne hii Julai 12 katika mji wa Arusha, nchini Tanzania ili kujaribu kuindoa nchi hiyo katika mgogoro unaoendelea. Kwa kikao hiki cha pili, Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa anaukutanisha utawala wa Bujumbura, upinzani uliolibaki Burundi, na baadhi ya wanaharakati wa vyama vya kiraia.

Nchini Burundi, hali ya usalama bado inadorora.
Nchini Burundi, hali ya usalama bado inadorora. Esdras Ndikumana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa wanasiasa wa upinzani na wale waliojitenga na chama tawala cha CNDD-FDD walio uhamishoni (CNARED), hawakualikwa. Baadhi ya vyama vya siasa kutoka muungano huo vimealikwa, lakini vimealikwa kama vyama vya kisiasa wala sio kwa niaba ya muungano.

Maandamano, mapigano na mashambulizi ni machache kwa sasa kuliko miezi iliyopita, lakini usalama bado unaendelea kudorora. Matumaini bado ni madogo.

Misako inayoendeshwa na polisi ikishirikiana na jeshi imekua ikifanyika kila kukicha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, hasa katika mji mkuu wa Bujumbura na viunga vyake, ikiwa ni pamoja na maeneo kulikoshuhudiwa maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza. Mashahidi na mashirika yasiyo ya kiserikali mara kwa mara wanalaani mauaji ya wafuasi wa upinzani na wakati mwengine wafuasi wa chama tawala wanalengwa, watu kukamatwa kiholeala. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaeleza kwamba utawala unataka kunyamazisha wapinzani.

CNARED bado haijatambuliwa ...

Serikali ya Burundi imeendelea kusema kuwa mashauriano tayari yameanza nchini Burundi baina ya Warundi. Tume iliyoteuliwa na utawala wa Bujumbura kwa minajili ya kuendesha maungumzo baina ya wadau walio ndani ya nchinii inaendelea na mazungumzo tangu miezi kadhaa, na kuweza kufikia katika uundwaji wa Katiba mpya.

Serikali inasema, wale utawala wa Bujumbura unawachukulia kama "magaidi" wametengwa katika mashauriano hayo. Serikali, hapo, inalenga muungano wa wanasiasa wa upinzani (CNARED Hakuna mazungumzo yanayowezekana: serikali ya Bujumbura inakataa katu katu kukaa kwenye meza moja na CNARED. Hii pengine ni kwa sababu hiyo mduluhishi ameamua kwa mara nyingine tena kualika mjini Arusha vyama mbalimbali kutoka CNARED, wala si ka niaba ya muungano huo.

Mwishoni mwa juma hili, msuluhishi katika mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa atawasilisha mpangilio wa mazungumzo kwa Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nje ya mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.