Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Tetemeko la ardhi Ufilipino: Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia watu watatu huko Mindanao
 • Pande zinazokinzana zaendelea tena na mazungumzo Jumatatu kujaribu kuiondoa Ireland ya Kaskazini katika mkwamo wa kisiasa
 • Mjumbe wa Marekani katika mazungumzo Stephen Biegun afutilia mbali msimamo wowote wa Korea Kaskazini lakini aacha mlango wazi kwa mazungumzo
E.A.C

Kifungo cha maisha jela dhidi ya viongozi 2 wa zamani Rwanda

media Rais wa Rwanda Paul Kagame akiambatana na mkew kwenye eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari katika maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994. REUTERS/Noor Khamis

Wakili Mkuu wa Serikali ameomba Jumatatu hii kifungo cha maisha jela dhidi ya mameya wawili wa zamani wa Rwanda, wanaotuhumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi katika kijiji chao mashariki mwa Rwanda mwezi Aprili, 1994.

Baada ya miezi miwili kesi hiyo ikisikilzwa mbele ya Mahakama ya Paris, Philippe Courroye amewataja Octavien Ngenzi, mwenye umri wa miaka 58, na Tito Barahira, mwenye umri wa miaka 65, kama wahusika muhimu katika mauaji ya kimbari yaliyotokea katika wilaya yao ya Kabarondo, akimtaja Octavien Ngenzi kama "kiongozi" na tito Barahira kama mfadhili wa mapanga.

Watu hao wawili, ambao wote wanakata kushiriki kwao katika mauaji ya kimbari, wamesikiliza hukumu dhidi yao huku wakipokea hukumu hiyo kwa shingo upande: Ngenzi "Yuda" ambaye hakufanya chochote kwa "kuzuia mauaji hayo" lakini "aliyasimamia". Barahira "mtekelezaji", ambaye alikua"akitoa maelekezo" na kushirikiana na wauaji, huku akibebelea mkuki mkononi.

"Wote hao walikua wauaji na wandaaji wa mauaji ya kimbari", wao, wanakabiliwa na mashtaka, "kukosa kukiri kosa lao, pamoja na kuomba msamaha" kwa kukana kosa lao hadi dakika ya mwisho.

Philippe Courroye amekumbusha kwamba watu hawa, waliokamatwa nchini Ufaransa wamehukumiwa chini ya uwezo wa mamlaka nzima ya mahakama za Ufaransa. Kesi hii ni ya pili kushughulikiwa nchini Ufaransa kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana