Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNICEF

UNICEF yakaribisha hatua ya viongozi wa polisi

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto duniani, UNICEF limesema kuwa limefurahishwa na hatua ya maafisa wa polisi mjini Bujumbura nchini Burundi ya kuwaachilia wanafunzi 6 hapo jana.

Kifo cha waziri wa zamani wa Rwanda katika gereza la Mpimba mjini Bujumbura, chazua maswali mengi, Machi 30, 2016.
Kifo cha waziri wa zamani wa Rwanda katika gereza la Mpimba mjini Bujumbura, chazua maswali mengi, Machi 30, 2016. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati hivi karibuni polisi nchini Burundi ilikamata kundi kubwa la wanafunzi wa shule ya sekondari kwa kosa la kuharibu picha ya rais wa nchi hiyo na kumtukana rais Pierre Nkurunziza, kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha miaka mpaka kumi jela.

Msemaji wa shirika hilo CHristophe Boulierac amethibitisha kuachwa huru kwa wanafunzi hao lakini amesema shirika hilo limeiomba serikali kuenda mbali zaidi na kuhakikisha haki za watoto zinheshimiwa nchini humo.

Hata hivyo bado kuna vijana miongoni mwa wanafunzi hao ambao wanaendelea kushikiliwa. Jana Jumatano vijana hao ambo ni wavulana na wasichana wameombea kifungo cha miaka kumi.

Mashirika yanayotetea haki za watoto nchini Burundi yamelaani hukumu hiyo, na kusema kuwa haki za watoto zinaendelea kukiukwa nchini humo.

Hayo yakijiri Mjumbe maalumu wa Marekani katika Ukanda wa Maziwa Makuu Periello, aliupokea jana Jumatano ujumbe mkubwa wa muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni CNARED nchini Ubelgiji. Mbali na hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi, ujumbe wa CNARED wamemuelezea Mjumbe huyo maalumu wa Marekani namna wanavyojiandalia kukutana kwa mazungumzo na msuluhishi wa mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.