Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI

EU kuendelea kusaidia wakimbizi wa Burundi

Umoja wa Ulaya umesema kuwa utaendelea kutoa misaada kwa raia wa Burundi waliokimbia machafuko nchini mwao na kupewa hifadhi makambini katika baadhi ya nchi jirani.

Wakimbizi wa Burundi wakikaa kwenye mtumbwi, karibu na ziwa Tanganyika kijijini Kagunga, upande wa Tanzania.
Wakimbizi wa Burundi wakikaa kwenye mtumbwi, karibu na ziwa Tanganyika kijijini Kagunga, upande wa Tanzania. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na RFI, msemaji wa tume ya umoja wa Ulaya, Alexandre Polack, amesema umoja huo umechukua hatua ya kutotoa misaada hiyo kwa wakimbizi kupitia kwa serikali, na sasa watapeleka kupitia mashirika yasiyo ya serikali yaliyoko Bujumbura na nje ya Burundi.

“Tunalazimika kutoa misaada ya moja kwa moja kwa wakimbizi. Nimesema ni watu wasiopungua laki mbili na sitini elfu; Tanzania pekee ikiwa na zaidi ya wakimbizi laki moja na arobaini elfu katika kambi ya Nyarugusu, ambayo imekuwa ni mojawapi ya kambi kubwa duniani, Kwa hiyo kutoa misaada namna hii, ni kuepukana na magonjwa ya milipuko”, amesema Alexandre Polack.

"Nchi zote za Umoja wa ulaya zimeamua tangu mwezi Machi kusitisha misaada kupitia serikali ya Burundi na tumeamua kwa pamoja kutoa misaada hiyo moja kwa moja kwa warundi. Na mwezi huu tutatoa kiasi cha Euro milioni 55 kwa raia walioko Burundi, na hii hatutaitoa kwa wakuu wa serikali bali tutapitia mashirika yasiyo ya kiserikali na yale ya kimataifa”, Alexandre Polack ameongeza.

Hatua hii inakuja ikiwa ni siku chache tu zimepita, toka umoja huo utangaze kusaidia wakimbizi wanaoishi kwenye makambi ya wakimbizi nchini Tanzania.

Burundi imekumbwa na machafuko tangu mwezi Julai baada tu ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu, muhula ambao upinzani na mashirika ya kiraia nchini wamekua wakisema kuwa ni ukiukwaji wa Katiba na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha, ambao ulikomesha machafuko yaliyodumu zaidi ya mwongo mmoja nchini humo tangu mwaka 1993.

Zaidi ya watu 270,000 walilazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia nchi jirani, kama vile Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, ...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.