Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO

Vuguvugu la mashirika ya kiraia laomba kualikwa katika mazungumzo

Vuguvugu la mashirika ya kiraia lililoandaa na kupanga maandamano dhidi ya kupinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza nchini Burundi “Halte au 3eme Mandat,” linaomba kualikwa katika mzungumzo ya Arusha, lakini limekataa kushirikishwa kwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko katika jopo la waandalizi.

Pacifique Nininahazwe, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu, pia muanzilishi wa vuguvugu "Halte au 3eme Mandat".
Pacifique Nininahazwe, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu, pia muanzilishi wa vuguvugu "Halte au 3eme Mandat". /kiyago.unblog.fr
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliotolewa na kusainiwa na wakili Vital Nshimirimana mjumbe mkuu wa Forsc, vuguvugu hilo limesema kufuatia mgongano wa maslahi uliopo juu ya ushiriki wa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko kwenye jopo la waandalizi, itakuwa vema kumuweka kando na mazungumzo hayo.

Vuguvugu hilo linalojumuisha mashirika kadhaa ya kiraia na ambayo viongozi wake wengi wanaeshi uhamioshoni kwa sasa, linaomba kuondolewa pia katika jopo la wandalizi Dokta Anthony Kafumbe.

Halte au 3eme Mandat limeomba mratibu katika mazungumzo Benjamin William Mkapa, kusaidiwa na wajumbe wataoteuliwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa

Mashirika hayo ya kiraia yanajidai kuwa ndio walioanzisha maandamano na wako tayari kutetea hoja zao na mkataba wa amani wa Arusha katika mazungumzo ya moja kwa moja yanayo tarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Wito pia umetolewa na mashirika hayo kwa msuluhishi kuhakikisha pande zote husika na mzozo zinashiriki huku wakibaini masikito yao kuona hawakufanya mashauriano na mratibu wa mazungumzo Benjamin William Mkapa.

Serikali ya Burundi inawatuhumu viongozi wa 3 wa mashirika hayo kuhusika katika jaribio la mapinduzi huku akaunti namba za baadhi ya mashirika yanayo jumuika katika vuguvugu hilo yakifungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.