Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-MAUAJI

Wakuu wawili wa zamani Rwanda kufikishwa kizimbani Paris

Miaka miwili baada ya jaribio la kesi ya kwanza nchini Ufaransa kwa mauaji ya kimabari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, kesi ya pili inafunguliwa Jumanne hii. Wakuu wawili wa zamani watafikishwa Jumanne hii mbele ya Mahakama ya mjini Paris baada ya kushtumiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994.

Sehemu ya mahakama katika jengo la mahakama mjini Paris, ambapo alihukumiwa Pascal Simbikangwa mwezi Februari 2014.
Sehemu ya mahakama katika jengo la mahakama mjini Paris, ambapo alihukumiwa Pascal Simbikangwa mwezi Februari 2014. © REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Octavien Ngenzi na Tito Barahira, ambao wanakanusha tuhuma hizo dhidi yao, wanashtumiwa kushiriki moja kwa moja katika mauaji ya mamia au hata maelfu ya Watutsi mwezi Aprili 1994 katika wilaya ya Kabarondo, hasa wakimbizi wa ndani walio kuwa walikusanyika katika kanisa wilayani humo, Mashariki mwa Rwanda.

Wawili hawa, ambao walipishana katika uongozi wa wilaya hii, watasikilizwa kwa muda wa wiki nane kwa "uhalifu dhidi ya ubinadamu" na "mauaji ya kimbari", kwa "kitendo kilichotekelezwa kwa watu wengina kwa muda mfupi" katika "utekelezaji wa mpango wenye nia ya kuangamiza" kabila zima la Watutsi.

Kesi ya mauaji ya kimbari inawekwa wazi sasa nchini Ufaransa: katika wilaya ya Kabarondo, mauaji yalimalizika kabla ya mwisho wa mwezi Aprili, baada ya waasi wa Kitutsi wa Rwanda Patriotic Front (RPF, kwa sasa madarakani) kuingia nchini humo. Wakati ambapo mauaji ya kimbari yaliyogharimu maisha ya watu wasiopungua 800,000, yalilizika mwezi Julai mjini Kigali.

Siku thelathini za kusikilizwa, vifungo 31 vya utaratibu na mashahidi wasiopungua 90 kwa muda wa wiki nane vyote hivyo vitakua vimekamilisha kesi hiyo. Kesi hii ni ngumu kutokana na kuzorota kwa afya ya Tito Barahira, ambaye atatimiza umri wa miaka 65 mwezi Juni, na ambaye anahudumiwa kimatibabu mara tatu kwa wiki.

Kwa sababu hiyo, kesi hiyo itakua ikifupishwa kila Jumatatu na Jumatano. "itabidi kesi hii ifupishwe mara kwa mara. "Mteja wangu anahitaji mara kwa mara kuhudumiwa kimatibabu na kujinyoosha sakafuni," alionya Bw Philippe Meilhac, mwanasheria wa Tito Barahira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.