Pata taarifa kuu

Polisi: "watu 49 walipoteza maisha Nairobi"

Watu 49 ndio walipoteza maisha wiki moja iliyopita wakati jengo la ghorofa sita lililopoporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, polisi ya Kenya imetangaza Jumapili hii.

Maporomoko ya jengo la ghorofa sita la tarehe 29 Aprili yaliwaua watu 49 mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Maporomoko ya jengo la ghorofa sita la tarehe 29 Aprili yaliwaua watu 49 mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Jengo hili lililojengwa karibu na mkondo wa maji, lilitangazwa na mamlaka kwamba lilijengwa eneo hatari, bila hata hivyo wamiliki wa jengo hilo kutojali onyo hilo.

Jengo hili la ghorofa sita liliporomoka baada mvua kubwa kunyesha usiku wa Aprili 29 katika kata ya watu wenye maisha duni ya Huruma, mjini Nairobi.

"Miili mingine saba ilitolewa katika vifusi vya jengo hilo mwishoni mwa juma hili", na kupelekea idadi ya watu waliopoteza maisha kuongezeka na kufikia 49, " Mkuu wa polisi, Yafethi Koome, amesema.

Tukio hilo la jengo kuporomoka ni la mwisho katika mfululizo wa matukio mabaya yaliyosababishwa na upanuzi wa haraka wa mji wa Nairobi ambapo ukiukwaji wa sheria ya mipango miji ni mara chache kuadhibiwa.

Wamiliki wawili wa jengo hili na maafisa watatu wa serikali walihojiwa Jumatano na polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.