Pata taarifa kuu
KENYA - UCHAGUZI

Kinara wa upinzani nchini Kenya aikosoa tume ya uchaguzi IBC

Kinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya, CORD, Raila Odinga ametaka kuongezwa kwa idadi ya mashine za kuandikisha wapiga kura ambazo zitatumika kwenye zoezi la kuorodhesha wapiga kura wapya, linaloanza Jumatatu ya wiki ijayo.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Matangazo ya kibiashara

Odinga amekosa maandalizi ya tume ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, na kudai kuwa kuna njama za kutosajili wapiga kura wengi zaidi kwenye mashine za BVR, na kwamba idadi ya kutumika kwa mashine 5756 peke yake kati ya eflu 15 zilizonunuliwa kunazusha hofu kuhusu utayari wa tume hiyo.

Odinga amesema IBC inatumia swala la fedha kama kisingizio ili kutosajili watu wengi, lakini pia haitowi muda wa kutosha kwa watu kujisaliji kama wapiga kura.

Odinga amesikitishwa kuona serikali ya rais Kenyatta inafanya hivyo kwa makusudi ili kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo IEBC imesisitiza kuwa mashine hizo zitatumika kama zilivyopangwa chini ya bajeti waliyotengewa na Serikali, na kwamba kila kaunti itakuwa na wafanyakazi wawili pekee watakaokuwa wakiandikisha wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.