Pata taarifa kuu
RWANDA - EAC

Mkutano wa viongozi wa Afya wa EAC kupanga mikakati kuzuia maradhi ya mlipuko

Viongozi wa afya kutoka Jumuiya ya Afrika mashariki pamoja na washirika waokatika jeshi la Marekani wanakutana jijini kigali nchini Rwanda ili kupanga mikakati ya pamoja kuzuia maradhi ya mlipuko ambayo yaweza kuwakumba sio tu wanajeshi lakini pia raia wa kawaida katika nchi za kikanda.

Wataalam wa Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wataalam wa Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
Matangazo ya kibiashara

Dokta Brigadia Jenerali Denis Janga wa kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania ambae anaongoza kikao cha siku mbili jijini Kigali nchini Rwanda amewaambia waandishi wa habari jijini Kigali hapo jana kwamba majeshi ya nchi 5 washirika yapo tayari kushikamana na washirika wengine wa sekta ya afya wa kikanda ili kuzuia kabia uwezekano wa maradhi ya mlipuko kuzikumba nchi hizi za kikanda.

Dokta Janga amesema wanakutana kila mwaka mara mbili ili kuzuia uwezekano wowote wa kutokea kwa maradhi ya mlipuko, lakini hadi sasa hakuna maradhi yoyote katika nchi za jumuiya hii, lakini na iwapo yataibuka wapo tayari kukabiliana nayo.

Mkutano huu unafanyika katika kipindi hiki kukiwa na kitisho cha mlipuko wa maradhio ya Zika katika bara la Amerika, na ambapo wajumbe mkutanoni wanajadili kuhusu njia ya kuepukana na maradhi hayo yasiwezi kuingia katika nchi hizi.

Brigadia Jenerali Denis Janga amesema ulimwengu mzima unatiwa wasiwasi na janga hili, hivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki ni sehem ya dunia hivyo wasiwasi pia unawakumba wahusika wa Afya, kwani yalishawahi kutokea majanga ya maradhi ya mlipuko huko Tanzania na Uganda.

Mkutano huo unaowakutanisha wakurugenzi wa sekta ya Afya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na washirika wao wa jeshi la Marekani ni katika azimio la kifungo nambari mbili cha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.