Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Serikali ya Marekani yaionya Rwanda kwa kuwanyima haki ya msingi wananchi wake

media Ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani

Serikali ya Marekani inaituhumu serikali ya Rwanda kuwakamata watu pasipo sababu na kuiomba serikali ya Kigali kuheshimu uhuru wa kujieleza, jambo ambalo limeilazimu serikali ya Rais Paul Kagame kujibu bila ya subira.

Katika taarifa iliyosomwa na Marie Harf, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, serikali ya rais Obama imeeleza wasiwasi wake kuhusu kutoweka kwa idadi kubwa ya watu katika mazingira tatanishi pamoja na vitisho vinavyoendelea dhidi ya waandishi wa habari.

Aidha, serikali ya Marekani inaiomba Rwanda kutoa maelezo kuhusu hatma ya raia wa rwanda waliokamatwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita na kuitaka iheshimu haki za binadamu kwa mujibu wa sheria za Rwanda na za kimataifa.

Onyo hilo limekuja saa chache baada ya kiongozi wa chama upinzani nchini Rwanda cha PS-Imberakuri Bernard Ntaganda kuachiwa huru ambapo ametumikia kifungo cha miaka minne jela kwa tuhuma za kujenga chuki, utengano na mifarakano nchini humo.

Akijibu tuhuma hizo za Marekani dhidi ya serikali, Louise Mukishiwabo Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda amewataka watu kuacha kutumia kila neno au tendo litakalowatia nguvu waasi wa kihutu wa FDLR pamoja na washirika wao na hivyo kuhatarisha maisha ya Wanyarwanda, na kwamba nchi yake haitasita kuchukua hatuwa madhubuti za kushughulikia tishio lolote kwa usalama wa Rwanda.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana