Pata taarifa kuu
KENYA-KIPCHOGE-RIADHA-DUNIA-MARATHON

Eliud Kipchoge aweka historia katika mbio za Marathon

Mkenya Eliud Kipchoge amekuwa mwanariadha wa kwanza duniani  kukimbia mbio za Marathon umbali wa Kilomita 42.2 kwa muda wa chini ya saa mbili.

Eliud Kipchoge, baada ya kushinda Marathon jijini  Viena, Austria, 12 Oktoba, 2019.
Eliud Kipchoge, baada ya kushinda Marathon jijini Viena, Austria, 12 Oktoba, 2019. Herbert Neubauer AFP
Matangazo ya kibiashara

Kipchoge mwenye umri wa miaka 34, aliweka historia hiyo baada ya kumaliza mbio za Marathon zilizofanyika jijini  Vienna nchini Austria kwa muda wa saa moja dakika 59 na sekunde 40.

Hata hivyo, rekodi hii haitambuliwi kama ya dunia kwa sababu mbio hizo hazikuwa za ushindani, lakini pia alitumia wanariadha waliomsaidia kuongeza mwendo.

Mwanariadha huyo alishangaliwa na maelfiu ya wapenzi wa riadha jijini Vienna wakiwemo raia wa Kenya waliokwenda kumshangilia huku wengine wakifutilia mbio hizo kupitia runinga kote duniani.

Baada ya kushinda mbio hizo, Kipchoge alisema amepata mafanikio makubwa na ameonesha kuwa, binadamu anaweza kufanya lolote, akiamua kufanya hivyo.

“Hii inaonesha kuwa, hakuna kisichowezeakana,” alisema.

“Sasa, mimi nimefanikiwa, natarajia kuwa wengine watafanya zaidi yangu, baada ya mafanikio haya,” aliongeza.

Bingwa huyo wa Olimpiki, anashikilia rekodi ya dunia kwa muda wa saa mbili, dakika moja na sekunde 39, aliyoweka jijini Berlin mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.